Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Jumatatu, Desemba 22, 2025, amefanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na urafiki wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), pamoja na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China.






