Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema shule ya kisasa ya sekondari Kitunda inatarajia kumalizika hivi karibuni ili wanafunzi waweze kuanza masomo.

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, amesema hayo Dar es Salaam jana katika ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Reuben Kwagilwa katika ziara yake ya kiserikali sekta ya elimu.

“Nawakikishia wazazi wa Kitunda na wazazi wa kata za jirani kukamilika kwa shule ya sekondari Kitunda Relini kabla mkataba wa ujenzi wake “alisema Mpogolo.

Mpogolo alisema ujenzi huo wa mkataba wake ulianza Septemba 2024 kwa mkataba wa miezi 18 lakini hadi kufikia sasa mradi huo umefikia asilimia 96 ya ujenzi wake .

Aidha alisema wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza fedha nyingi katika miradi ya sekta ya elimu Wilayani Ilala ambapo alisema mradi huo umetekelezwa ndani ya mwaka mmoja .

Alisema kuwa inathibitisha matumizi mazuri ya muda na thamani ya walipa kodi kwa kazi kwenda kwa wakati .