Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuzindua Meli ya kisasa ya MV. New Mwanza iliyokuwa ikijengwa katika Bandari ya Mwanza Kusini.
Hayo yamebainishwa Leo Alhamisi Januari 22, 2026 na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kukamilika kwa mradi huo.
Amesema uzinduzi huo utafanyika kesho Ijumaa Januari 23, 2026 huku akieleza kuwa Meli hiyo ni kubwa kuliko zote katika ziwa Victoria kutokana na kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200,Tani 400 za mizigo,magari madogo 20 pamoja na magari makubwa 3.
“Meli hii imeundwa kwa viwango vya kimataifa na imegharimu zaidi ya bilioni 120 na ina urefu wa mita 92.6 upana mita 17”, Amesema Prof.Mbarawa
Mwisho aliwakaribisha wananchi wa Mikoa ya Mwanza,Kagera,Mara na viunga vyake kuhudhuria na kufuatilia ziara hiyo kwaukaribu.



