Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa fedha za miradi ya maendeleo sio siri, na. watendaji wa Serikali wanapaswa kuacha ubinafsi kwenye matumizi ya fedha hizo.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa fedha hizo zinazotokana na kodi za wananchi, hivyo zinapaswa kwenda kutekeleza miradi kama ilivyokusudiwa. “Hatuwezi kufanya ustaarabu kwa mtu anayetafuna fedha za umma za umma, Rais Dkt. Samia anatafuta fedha za miradi halafu anatokea mtu anaziiba, hii haiwezi kukubalika”

Amesema hayo leo Jumamosi (Februari 21, 2026) alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bomang’ombe hadi Kikavuchini kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 25.7.