Takriban watu 11 wamejeruhiwa katika shambulizi la Ukraine katika eneo la Urusi lililo na utawala wake wa ndani la Jamhuri ya Udmurtia, linalojulikana kwa sekta imara ya uundaji wa vifaa
Katika chapisho kwenye mtandao wa Telegram akiwa mjini Izhevsk, waziri wa afya wa Jamhuri hiyo Sergei Bagin, amesema watu watatu walipelekwa hospitalini .
Ripoti za mitandao ya kijamii ambazo hazijathibitishwa zimesema kuwa kiwanda muhimu cha silaha huko Votkinsk, takriban kilomita 50 kaskazini-mashariki mwa Izhevsk, ambacho hutengeneza makombora ya Iskander na Oreshnik, huenda kililengwa.
Wakazi wa eneo hilo, ambalo liko upande wa magharibi wa Milima ya Ural, walichapisha picha mtandaoni zinazoonyesha moto na uharibifu wa majengo. Akaunti zingine zilidai kuwa kituo cha utengenezaji wa roketi kililengwa, ingawa hapakuwa na uthibitisho rasmi.
Mapema, gavana wa Jamhuri hiyo ya Udmurtia Aleksandr Brechalov, alisema kituo ambacho hakijajulikana kililengwa kwa droni, na kuripoti kuhusu uharibifu na majeruhi.
Hakutoa maelezo zaidi, kama vile eneo kamili la shambulizi.

