Na Heri Shaaban, JamhuriMesia, Dar es Salaam

WANAWAKE wa Jeshi la Zimamoto Uokoaji Uwanja wa Ndege (JNIA) wilayani Ilala, Dar es Salaam wametoa vyakula vya misaada na mahitaji mbalimbali kwa watoto wa Mazingira Magumu katika kusherekea siku ya Wanawake Duniani kituo cha watoto wenye mahitaji maalum Zili House Children Care.

Akikabidhi vyakula hivyo kiongozi wanawake Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Uwanja Ndege JNIA Mrakibu Msaidizi Jeshi la Zimamoto la Uokoaji,Theresia Tengia amesema katika wiki hii ya siku ya Wanawake Duniani wao wanawake wa Zimamoto Uwanja Ndege JNIA wanatembelea vituo vya watoto wa makundi maalum kutoa misaada mbalimbali sambamba na kufanya kazi za kijamii.

“Sisi Wanawake wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Uwanja Ndege JNIA leo tunadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwa kutembelea vituo vya watoto wa makundi maalum na kutoa misaada yetu ni sehemu ya furaha tunashiriki nao pamoja” amesema Theresia

Mrakibu wa Msaidizi wa Jeshi Zimamoto na Uokoaji Uwanja Ndege JNIA Therea amesema katika kazi mbalimbali za kijamii walizofanya wiki hii ya Siku ya Wanawake Duniani sambamba na kufanya kazi za kijamii shule ,hospitalini .

Amesema Jeshi la Zimamoto linashughulika na kazi mbalimbali wakati wa majanga katika kusaidiana jamii ikiwemo kuwaokoa sehemu mbalimbali katika matukio.

Pia Maafisa hao wa Jeshi la Zimamoto Kituo cha JNIA wamefanikiwa kumtembelea Bi. Asia Chande -Tandale Uzuri mwenye changamoto ya maradhi ya mifupa na kufanikiwa kukabidhi misaada mbalimbali ya kijamii