Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Kituo cha Sheria na Usuluhishi cha CRC kimesema migogoro ya mahusiano na elimu ya afya ya uzazi ni changamoto kwa wanandoa na vijana nchini.
Akizungumza na Jamhuri mara baada ya kikao cha mkutano wa mwaka wa kituo hicho ,mratibu wa kituo hicho ,Gladness Munuo amesema kituo hicho kimefanya kazi kubwa ya usuluhishi mwaka 2024/2025 miongoni
inayo ongoza ni ya mahusiano.
Amesema wanandoa wengi kwa sasa hasa wanaume wamekuwa na changamoto za
kuwaachia malezi wanawake peke yao ,kitu ambacho kinawafanya wanawake
kuhangaika na watoto na kuomba msaada katika kituo hicho.
Amesema katika mkutano huo walizungumzia maswala kadhaa ya kuimarisha kituo hicho , ili kuendelea kutoa huduma za kisheria na ushauri nasihi
ambapo kwa sasa kinatoa elimu katika maswala mbalimbali yanayo hakikisha mwanamke anapata elimu ili aweze kujitetea sambamba na kufahaumu mipaka yake ikoje katika jamii.
‘’Katika mkutano tulijadili maendeleo yaliyofanyika katika kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa mwaka 2025 ,hali ya migogoro bado inayoongoza ni ya mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume pengine ni kutokuelewa au kuto zingatia sheria na watu kukosa hofu ya
Mungu .

Amesema kituo kimekua kikifanya jitihada za kuhakikisha elimu inafaika kwa jkamii kwa kuhakikisha wanashirikiana na vyombo mbalimbali vya habari ili kutoia elimu kwa watu waweze kuelewa sharia mbalimbali
‘’Tumekuwa tukiwapa elimu na ushauri na kutatua migogoro ambapo kwa sasa takwimu zetu zinaonyesha , migogoro ipo kwa wanaume wengi wamekimbia familia kwa hiyo tumejaribu kuwa kutanisha baadhi ya familia na kusuluhisha sambamba na kukutana na watunga sera ambao ni
wabunge kubadilishana mawazo nini kifanyike’’amesema
Katika maswala wa sera na sheria tumekuwa tukitekeleza mradi iweze kufanyiwa marekebisho ya uzazi salama ,kwasababu vijana wanahitaji elimu kwani bila muongozo hawawezi kuwa bora huko mbeleni kwani wao watakua wanajiamulia tu bila kuongozwa .
CRC tunataka wajue nini kinachojili katika maswala ya uzazi ,ambapo mara nyingi wamekuwa wakipotea sana ,ila tunaamini kuwa kupitia semina mbaimbali wataweza kubadilika na kwenda katika mkondo sahihi namba zetu za ushauri wa msaada wa kishria na msaada ni 0680100998’’amesema
Amesema wanatoa elimu mbalimbali hasa afya ya uzazi kwa vijana hasa wanafunzi ili dunia iwe salama kwa kukomesha ukatili wa kijinsia na hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu tunawapatia elimu kwasabbau wengi
wapo kwenye mahusiano na hawajui cha kufanya matokeo yake wanatumia mbinu mbalimbali wakati mwingine wamekua wakikiuka maadili wanajiumiza hasa pale anapohitaji kuwa na mahusiano ya kweli yeye mwenyewe anakwama kutokana na vitu ambavyo amewahi kutumia huko nyuma .
Ameomba serikali tuendelee kuwa na sera rafiki kwa vijana tunashukuru sasa kuna wizara tunaamini itawalinda na kutatua
changamoto zao.


