N Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limepongezwa kwa mafanikio na kuwaleta wadau mbalimbali pamoja na watoto yatima na kuwapatia Iftar .

Akizungumza katika hafra ya Iftar na dua iliyoandaliwa na TASAC kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere kama mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amewapongeza TASAC , kwa kuimarisha ushirikiano na wadau kwa kuwaleta pamoja kwenye iftar lengo likiwa ni kudumisha urafiki, mshikamano na umoja katika sekta ya usafirishaji majini.

Amesema Mwezi mtukufu wa Ramadhani, unafundisha kujenga mahusiano mema
kwa kuimarisha mshikamano na kutafsiri umoja kama walivyofanya TASAC .

Mbarawa amesema katika sekta ya usafiri majini, mshikamano, ushirikiano kati ya serikali ,Taasisi na wadau wa sekta binafsi ni jambo la msingi katika kuhakikisha inakuwa na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa letu.

‘’Napenda kutumia fursa hii kutambua mchango mkubwa, unao tolewa na TASAC katika kusimamia na kuthibiti usafiri majini.

Shirika lina jukumu muhimu la kuhakikisha, usalama wa vyombo vya majini abiria na mali zao sambamba na kuzibiti uchafuzi wa
mazingira baharini na kwenye maziwa unaotokana na shuguhuli mbalimbali za meli .

Kusimia usajili wa meli kuzibiti huduma za usafiri majini, ikiwemo bandari na huduma za uwakala wa forodha kwa shehena mahususi zenye maslahi kwa taifa sambamba na kuhakikisha uzingatiaji wa sheria na kanuni za kimataifa zinazohusu usafiri wa majini zinafuatwa.’’amesema.

Aidha pamoja na Majukumu haya TASAC, imeendelea kuchangia kuimarisha usalama wa usafiri majini kuongeza ufanisi katika shughuli za bahari pamoja na kusadia kukuza biashara na zinazotegemea njia za usafiri majini.

‘’Serikai chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka msisistizo mkubwa katika kuimarisha miundo mbinu ya uchukuzi ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Katika sekta ya usafiri majini, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbali kuboresha bandari na kuimarisha usalama wa vyombo vya majini

Katika muktadha huoTASAC ina nafasi kubwa ya kuhakikisha, shughuli za usafiri majini zinaendeshwa kwa kuzingatia viwango vya taifa na kimataifa ili kulinda usalama watu wetu na mazingira ya
majini’’amesema

Amesema Serikali katika sekta ya uchukuzi ,imejidhatiti kulinda Wananchi na mali zao wanakuwa salama kwa kuimarisha mifumo ambayo hata ikitokea dharula kunakuwa nauokozi waharaka .

Ametoa wito kwa wadau wa sekta ya usafiri majini, kuendelea kushirikiana kwa karibu na TASAC kwa kuzingatia sheria ,kanuni na
taratibu zote zinazohusu shughuli za usafiri majini .

‘’Ushirikinano huu ni muhimu katika kuhakikisha ,tunakuwa na sekta yenye ufanisi usalama na inayochangia kikamilifu maendeleo yetu11’amesema

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mohamed Salum amehimiza umoja na mshikamano
miongoni mwa wadau na wafanyakazi wa TASAC walio hudhulia iftar kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa karibu na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma.

“Kukutana pamoja katika mwezi huu wa Ramadhani ni fursa nzuri ya kusherehekea mafanikio ya kazi na malengo yaliyofikiwa na TASAC .

Huu ni wakati mzuri wa kutathmini mafanikio yaliyopatikana nakujivunia juhudi za pamoja za wafanyakazi na wadau, huku tukiboresha
umoja na mshikamano wetu.

Katika hafra hiyo TASAC iliwakutanisha wadau mbalimbali pamoja na watoto yatimakutoka hisani orphanage centre kwa kuwapatia chakula na mahitaji mengine muhimu kwa ajili ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid.