Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka Mitano ya Kifo cha Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, itakayofanyika kesho tarehe 17 Machi 2026 Chato mkoani Geita.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita, leo tarehe 16 Machi 2026.