โข Akagua na kuipongeza Serikali kuchukua hatua za haraka
โข Daraja hilo sasa kukamilika
Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kigamboni
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. ๐๐ฎ๐ฟ๐ฎ๐ป ๐ฆ๐ฎ๐ป๐ด๐ฎ ameipongeza Serikali kwa hatua za haraka za kurejesha mawasiliano katika Daraja la Nguva ambalo liliathirika na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha changamoto ya uvukaji wa wananchi kwenda upande wa pili.
Akizungumza muda mfupi baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati huo, amsema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na TANROADS wamechukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wanavuka na kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Daraja hilo linaunganisha mawasiliano ya Kata za Somangila na Kimbiji katika eneo la Mwongozo na Gezauole.
โSerikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha mawasiliano yote kwa ujumla yanarejea ambapo hadi kufikia muda huu tayari magari madogo, bajaji, pikipiki na waenda kwa miguu wameweza kuvuka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hii ni hatua nzuri na tunaipongeza Serikali kwa kutatua changamoto hii kwa haraka,โ alisema Mhe. Sanga.
Ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuzingatia taarifa na tahadhari zinazotolewa au kutangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza hasa kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.
Kwa upande wake Meneja TANROADS mkoa wa Dar es salaam Injinia Lazeck Kyamba, amesema jitihada za kujaza kifusi ili kufikia usawa wa daraja jipya linalojengwa zinaendelea ili mawasiliano ya njia hiyo yarejee kama awali.
Ujenzi wa Daraja jipya la Nguva unaenda sambamba na Daraja la Kibugumo ambapo gharama zake ni Tsh Bilioni 9.2 fedha zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป.





