Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo Jumatano, Septemba 16, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Barrick kuhusu namna bora ya uendelezaji wa migodi nchini.
Ujumbe wa Barrick uliongozwa na Afisa Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Barrick, Bw. Woo Lee, ambaye aliambatana na Makamu wa Rais wa Masuala ya Kimataifa wa Barrick, Bw. James Ratchford, pamoja na Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Bw. Melkiory Ngido.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna bora ya kuendeleza shughuli za uchimbaji madini, pamoja na kuangalia fursa za kuimarisha ushirikiano na kuongeza manufaa yatokanayo na sekta ya madini kwa uchumi wa Tanzania.






