Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia Dar es Salaam

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa pili wa Afrika na nchi za Ghuba (GCC Plus), utakaolenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya uhamaji wa wafanyakazi,ajira na mahitaji ya soko la ajira kati ya nchi za Afrika na Mataifa ya Kiarabu.

Mkutano huo utafanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu nakwamba utawakutanisha wanachama wa Umoja wa Afrika(AU), nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC), ambazo ni Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Kuwait, Oman na Bahrain, pamoja na Jordan na Lebanon.

Hayo yamesemwa leo Septemba 28,2026 na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,na Mahusiano Deus Sangu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Sangu amesema Mkutano huo unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja kuhusu uhamaji salama, wenye tija na unaozingatia haki za wafanyakazi, pamoja na kukuza fursa za ajira, hususan kwa vijana.

Amefafanua kuwa Mkutano wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika jijini Doha, Qatar, Mei 21 na 22, mwaka 2024, ukihudhuriwa na nchi 43, zikiwemo nchi 25 za Afrika, nchi za GCC pamoja na Jordan na Lebanon, kwa pamoja zikijulikana kama GCC Plus.

“Tanzania ilishiriki katika mkutano huo wa kwanza ambao ulihusisha majadiliano yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika na nchi za Kiarabu katika masuala ya uhamaji wa wafanyakazi.”amesema

Ameongeza kuwa Mkutano huo ulihitimishwa kwa kupitishwa kwa Azimio la Doha(Doha Declaration),lililoweka msingi wa kuendeleza majadiliano na ushirikiano kati ya pande hizo.

Halikadhalika amesema Tanzania imepata nafasi ya kuwa nchi ya pili kuwa mwenyeji wa mkutano huo, ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili, na kwa mara ya kwanza kufanyika katika bara la Afrika.

“Moja ya maeneo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni kuimarisha uhamaji wa wafanyakazi kati ya nchi, ikiwemo makubaliano ya uhamaji (Migration Agreements), ujuzi wa wafanyakazi, mahitaji ya soko la ajira na uanzishwaji wa mifumo ya kusaidia uhamaji salama na wenye tija” amesema

Kwa mujibu wa Sangu mkutano huo utajadili namna ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia, mabadiliko ya mahitaji ya soko la ajira pamoja na kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira la sasa na la baadaye.

Kwa Tanzania, mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa ya kimkakati ya kuimarisha nafasi ya nchi katika mijadala ya kimataifa kuhusu uhamaji wa wafanyakazi, kubainisha fursa za ajira ndani na nje ya nchi, kulinda haki za wafanyakazi na kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika na GCC Plus.

Pia, mkutano huo unatarajiwa kuongeza ushindani wa wafanyakazi wa Tanzania katika soko la ajira la kimataifa na kuchangia katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo ya taifa.

Kwa ujumla, mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika na GCC Plus katika masuala mbalimbali ya uhamaji wa wafanyakazi, huku ukigeuza makubaliano na majadiliano yaliyopo kuwa hatua za vitendo na matokeo yanayopimika.

Kupitia ushirikiano huo, Tanzania inatarajia kuona fursa zaidi za ajira kwa Watanzania, hususan vijana, huku ikiweka mkazo katika uhamaji wa wafanyakazi ulio salama, wenye haki, tija na unaozingatia mahitaji ya nchi na soko la ajira.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, inaamini kuwa mkutano huo utaimarisha ushirikiano na washirika wa kimataifa na kufungua fursa zaidi za ajira kwa Watanzania.

Nimeweka “uhamaji wa wafanyakazi” badala ya “maji ya mfukozi,” kwa kuwa kutokana na muktadha wa Migration Agreement, soko la ajira na haki za wafanyakazi, inaonekana hiyo ndiyo istilahi iliyokusudiwa.