Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa sana taarifa ya kifo cha mwanafunzi Raiyan Hemed Amour (15) wa kidato cha kwanza katika Skuli ya Sekondari Kizimbani, Pemba ambae kimetokea wakati mwanafunzi huyo akirudi skuli.
Mwanafunzi huyo aliripotiwa kupotea na baadaye kupatikana akiwa amefariki.
Wizara inalaani kwa nguvu zote kitendo hiki cha kikatili na kisicho cha kibinadamu, na inatoa pole na rambirambi za dhati kwa familia, ndugu, jamaa, walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla kutokana na msiba huu mzito.
Wizara inaviomba vyombo Vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina na kwa haraka ili kubaini wahalifu pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
Wizara pia inatoa wito kwa jamii kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote muhimu zinazoweza kusaidia katika uchunguzi
Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya mtoto wetu mpendwa mahali pema peponi na awape familia na wote walioguswa na msiba huu nguvu na subira katika kipindi hiki kigumu.



