Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Leo 7 Oktoba 2026, amewasili Nchini Uingereza ambapo atakuwa mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania nchini Uingereza.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu pia ataongoza ujumbe wa Tanzania kukutana wadau, wawekezaji na viongozi wa kampuni mbalimbali katika sekta za madini, benki, Teknolojia, usafirishaji na miundombinu, kwa lengo la kuimarisha na kutangaza fursa za Biashara na Uwekezaji.