Kesho tarehe 14, Oktoba , 2026 mama yetu mpendwa Maria Nyerere amefanya uzinduzi wa daraja la Mto Kasitu lililogharimu kiasi Cha Shilingi bilioni 4.7 chini ya Wakala wa Barabara za Mijini Vijiji (TARURA) .

Mama Maria Nyerere amewapongeza wananchi wa Kalambo kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa Serikali katika kudumisha amani na mshikamo ambavyo ni chachu ya kuleta maendeleo katika nchi.

Katika uzinduzi wa mradi huo wa daraja amesindikizwa na viongozi akiwemo Waziri wa TAMISEMI, Riziki Shemdoe, Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Hamida Mussa Khamis, Rashid Hadid Rashid Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hajat Silafu Jumbe Maufi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa pamoja na viongozi mbalimbali.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania alimpa Mama Maria Nyerere kwa heshima Jina la Daraja hilo na kulizindua leo.