Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Shirika la Usafiri wa Baharini la Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Kaskazini (MOESNA), utakaofanyika Oktoba 15, 2026, katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha takribani mawaziri 26 wanaoshughulikia masuala ya uchukuzi na lojistiki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi za baharini za kimataifa na kikanda.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Naibu Waziri waa Uchukuzi Davidi Kihenzile Leo Oktoba 13, 2026 Jijini Dar es Salaam, amesema mkutano huo unakwenda kutajadili mikakati ya kuboresha shughuli za biashara miongoni mwa nchi wanachama, kwa kuimarisha sekta ya uchukuzi na lojistiki kupitia usafirishaji wa majinai .

“Ajenda kuu ya mkutano huu ni kukuza biashara kupitia upanuzi na uimarishaji wa huduma za usafirishaji wa mizigo na abiria kwa njia ya bahari.” amesema Naibu Waziri

Hatua hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya uchukuzi wa baharini na kuongeza fursa za biashara kati ya nchi za Afrika Mashariki, Kusini na Kaskazini.

Uenyeji wa mkutano huo unaipa Tanzania fursa ya kushiriki katika majadiliano ya kikanda kuhusu maendeleo ya uchukuzi na lojistiki, maeneo muhimu katika kurahisisha biashara na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi baina ya nchi za Afrika.

Mkutano huo unafanyika katika kipindi ambacho Tanzania inaendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha sekta ya uchukuzi na lojistiki chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Na Mwandishi Wetu — Dar es Salaam

Hata hivyo amesema Tanzania tayari mipango imeshafanyika imeteuliwa kujengwa Chuo kiku cha wa Majina.Aidha Mkutano huo ohudhuriwa Mawaziri 26 wa Uchukuzi Afrika na Atakayefungua ni Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba

Kwa upande wake katibu mtendaji wa MOESNA Kassim Mpaata amesema .Nchi za Afrika Mashariki, Kusini na Kaskazini mwa Afrika zimepitisha mchakato wa kujenga Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Bahari (Regional Maritime University) kitakachohusisha nchi zote za kanda hizi.

Mchakato huu pia umelenga kuwa na makao makuu ya chuo hicho nchini Tanzania, pamoja na kuwa na makao madogo au vituo katika nchi zote zinazoshiriki.

“Kutokana na kuwepo kwa tofauti za kiwango cha mafunzo ya bahari katika nchi mbalimbali, nchi hizi zimekubaliana kuhitaji kituo cha ubora cha kikanda (Regional Centre of Excellence) kitakachofuata viwango vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa na Serikali ya Tanzania. ” Amesema Mpaata

Hata hivyo amebainisha kuwa Mpango huu tayari umepata uungwaji mkono kutoka kwa nchi mbalimbali ikiwemo Kenya na zingine zilizotangaza utayari wao wa kuchangia.

Gharama za ujenzi na uendeshaji wa chuo hichi zitagawangwa na nchi zote shiriki, huku Tanzania ikiongoza mchakato huo.