Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi tarehe 15 Oktoba 2026, amehudhuria hafla rasmi ya ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Dunia kuhusu Bioanuai (COP17), uliofanyika katika Kituo cha Michezo na Matamasha cha Karen Demirchyan, jijini Yerevan, Armenia.
Rais Dkt. Mwinyi anashiriki mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkutano huo umewakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na wakuu wa ujumbe kutoka nchi mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha juhudi za kimataifa za uhifadhi wa bioanuai na kuharakisha utekelezaji wa malengo ya kuhifadhi na kurejesha mazingira ya asili ifikapo mwaka 2030.









