Na Anthony Mayunga, JamhuriMedia, Serengeti
Miongoni mwa mambo yanayolitesa taifa letu ni baadhi ya viongozi na watendaji kushindwa kutekeleza wajibu wao, matokeo yake, jamii huathirika na serikali hutumia fedha nyingi kutibu madhara ambayo yangeweza kuzuilika.
Uchafu huchangia magonjwa, gharama za matibabu na vifo. Serikali hununua dawa, lakini wakati mwingine wahusika husubiri hadi Rais atoe maelekezo ndipo wachukue hatua, huu ni udhaifu wa usimamizi unaopaswa kurekebishwa.
Tatizo si taka, bali mfumo wa udhibiti. Tanzania Bara inazalisha takribani tani 689,144 za taka ngumu kila mwezi, kati yake tani 339,095.2, sawa na asilimia 49.2, hukusanywa, huku zaidi ya tani 325,000 zikifikishwa maeneo maalumu ya kutupia taka.
Hii ina maana kiasi kikubwa cha taka hubaki nje ya mfumo rasmi. Kwa hiyo tatizo si usafi wa miji pekee, bali ni afya ya wananchi na uwezo wa taasisi kutekeleza majukumu yake.
Kwa miaka mingi, tumekuwa tukiwaelekeza wananchi wasitupe taka ovyo, wasafishe mazingira na washiriki kampeni za usafi. Ujumbe huu una umuhimu wake, lakini hauwezi kutatua tatizo bila mfumo wa uhakika wa kukusanya, kusafirisha na kutupa taka salama.
KWA HABARI ZA KINA ZAIDI SOMA GAZETI LA JAMHURI LA OKTOBA 20 – 26, 2026


