Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

WATAALAM wa fani ya Malikale wa Tanzania na Kimataifa wametakiwa waendelee kufanya tafiti zaidi nchini Tanzania kuibua maeneo zaidi yenye Urithi wa Masalia ya Kale ili jamii iweze kunufaika na matokeo ya tafiti zao.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili nchini Balozi Dkt. Pindi Chana wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa wataalam wa Fani ya Masalia ya Kale, Jijini Arusha.

Balozi Dkt. Pindi Chana amesema matokeo Chanya ya kazi nzuri ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuibeba sekta ya Utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour, yawe kichocheo cha ongezeko la tafiti nyingi zitakazo ibua maeneo mapya ambayo yatavutia watalii zaidi.

Nchi zaidi ya 15 zinahudhuria mkutano huo, zikiwemo, Marekani, Canada, Uingereza, Ujerumani, Hispania, Italia, Uswisi, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, India, Afrika Kusini, Ethiopia, Kenya ,Tanzania na Uganda.

Aidha kufanyika Kwa mkutano huo nchini Tanzania kunatoa fursa kwa watalaam hao kutembelea maeneo mbalimbali yenye historia kubwa ya Masalia ya Kale likiwemo eneo la Olduvai Gorge na Laetoli ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

By Jamhuri