Watanzania watakiwa kuwa waaminifu

Na Aziza Nangwa,JamhuriMedia,Dar

Balozi wa Tanzania Nchini Saudi Arabia Ali Mwadini amewataka watanzania kuwa waaminifu, katika ufanyaji biashara zinazoenda nje ya nchi.
Mwandini amesema kama watanzania wanazingatia kuwa waaminifu katika biashara,ni wazi wataweza kumuhifadhi mteja wa bidhaa lakini ukimfanyia visivyo utampoteza.

Balozi wa Tanzania Nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini akizungumza katika Kikao na wawekezaji kutoka nchini Saud Arabia

“lazima kila mfanyabiashara afanye kwa uaminifu ili asiwaangushe ,watanzania wengine kwenye sekta hiyo ya biashara watanzania wanaweza kuzingatia Ujazo wa bidhaa, ingawa zinagombaniwa na masoko ni Ubora wa bidhaa”amesema Mwandini

Kitu cha kuzingatia lazima mfanyabiashara ,uzalishe kwa ubora kuanzia uchakataji, Usafirishaji, uhifadhi pamoja na ufungashaji kabla ya kupelekwa bidhaa zako kwenye soko.

Amesema kwa sasa Saudi Arabia kwa sasa bado ina uhitaji wa bidhaa za kilimo, ufugaji na uvuvi bado yanasoko na hayana ukomo, kwani nchi hiyo aina uwezo wa kujaza soko la ndani na kukidhi mahitaji yote ya wakazi wake.

Mwandini amesema kwa sasa nchi hiyo bado inaagiza bidhaa kutoka nje kwani mahitaji ni makubwa kwani inawakazi zaidi ya milioni 35, na wanazalisha chakula kwa asilimia 5 na asilimia 95 wanaagiza kutoka nchi mbalimbali .

“Wawekezaji waliokuja wamekuja nchini kukamilisha, taratibu za uwekezaji na kukuza mahusiano ya kiuchumi baina ya Tanzania na Saudi Arabia”amesema Mwandini.

Mwadini amesema Tanzania imepata kibali cha kusafirisha nyama pamoja na mifugo hai, kuipeleka nchi ya Saudi Arabia kwaajili ya kukuza biashara na uchumi kupitia fursa hiyo.

Revocatus Rasheli ni Kaimu Mkurugenzi Uhamasishaji amesema nchi ya Saudi Arabia imewekeza nchini , miradi 13 ambayo inagharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 55.2 kwenye sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi na kutoa ajira kwa vijana kupitia fursa hizo.

Rasheli mesema katika kutekeleza mkakati wake wa miaka mitano imeweka kipaumbele, kwenye uwekezaji wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ,ambapo kwa sasa wako katika kuongeza Viwango vya uzalishaji katika maeneo hayo ili kuwavutia wawekezaji zaidi.

Amesema wawekezaji wameweza kupata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali kutoka bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko (CPB), pamoja na ranchi ya taifa (NARCO) ili waweze kuangalia maeneo ambayo wawekezaji hao wanaona wanaweza kufanya uwekezaji.

Amesema katika kuona fursa za uwekezaji wawekezaji hao, wanatarajiwa kuwekeza katika katika ufugaji ,kilimo na uvuvi.