Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Abdullah Al Sharyan akizungumza na wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini humo ambao wako katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akimwelezea Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa ziara yake aliyoifanya leo JKCI kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo ya matibabu itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.Picha na Khamisi Mussa
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akisalimiana na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo maalum itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.

By Jamhuri