Na Mwamvua Mwinyi,JamhuriMedia, Pwani

Mkoa wa Pwani unajivunia uwekezaji mikubwa ya kimkakati ambayo italeta Mapinduzi makubwa tangu Uhuru mwaka 1961 ikiwemo Reli ya kisasa (SGR) inayopita Mkoani humo kwa kipande kinachoanzia Dar es salaam -Morogoro chenye km.300.

Mradi mwingine ni ule wa bandari kavu Kwala unaotarajiwa kuanza kazi January 2023 pamoja na mradi mkubwa wa Nishati ya umeme stiglers uliopo wilayani Rufiji ambao unakwenda kuondoa changamoto ya upungufu wa umeme nchini.

Katibu Tawala mkoani Pwani Zuwena Omari akizungumza katika Kongamano la miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara lililofanyika Disemba 9, 2022 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kibaha alieleza maendeleo hayo ni makubwa ukitofautisha na miaka ya nyuma .

Aidha alieleza ili kuendelea zaidi kiuchumi na kimaendeleo lazima kuwe na amani na umoja.
Hata hivyo Zuwena alifafanua, kila mmoja kwa nafasi yake ndani ya jamii awajibike na kujitambua,kuvumiliana ili kuendeleza amani na utulivu uliodumu kwa miaka 61.

Akielezea mada ya miundombinu Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Pwani ,(TANROADS) Mhandisi Baraka Mwambage alieleza wamefanya mabadiliko katika mradi wa kimkakati wa Daraja la WAMI lililojengwa kipindi cha nyuma mwaka 1959 kabla ya Uhuru na Sasa limekuwa la kisasa na kupunguza changamoto za ufinyu uliokiwa ukisababisha ajali za mara kwa mara.

Alisema , pia kwasasa wanajipanga kuboresha barabara ya Kibaha-Kisarawe kwa kiwango Cha lami yenye km.19 na sasa wapo hatua ya usanifu.

Baraka alieleza kwa miaka yote barabara hiyo ni ya vumbi hivyo kwasasa inaboreshwa kuendana na wakati na maendeleo yaliyopo.

Pia upanuzi wa barabara ya njia nane na mwendo Kasi kutoka Kimara -Kibaha unaendelea na ili kuondoa msongamano barabara ya Mbagala rangi tatu-Kisemvule-Vikindu km 4 kwa njia nne usanifu unafanyika ili kuanza maboresho ya barabara hiyo.

Kuhusu mada ya afya Mganga Mkuu wa mkoa Dkt.Gunini Kamba alieleza mwaka 61 mkoa wa Pwani ulikuwa na hospital moja ya Tumbi , kwasasa zipo tano katika wilaya tano ,vituo vya dharura vitano ,vituo vya afya 437 ambapo vingine vinatoa huduma ya upasuaji wa dharura.

“Vituo kumi vimejengwa kwa fedha za tozo na vipo kila Halmashauri”alieleza Gunini.
Alieleza kulikuwa na changamoto ya uhaba wa watumishi Ila sasa kuna watumishi 2,257 na wapya 359.

Upande wa sekta ya elimu ,ofisa elimu mkoa Sara Mlaki alieleza , 1961 kulikuwa na shule za msingi 172 sasa zipo 720 kati ya hizo 605 ni za Serikali, walimu wa shule za msingi walikuwa 923 Sasa 6,568,nyumba za walimu 131 za sasa 2,296.

Sekondari kipindi hicho wanafunzi walikuwa 393 sasa ongezeko ni 32,331, nyumba za walimu Sekondari 17 sasa 738.

Mlaki alieleza kwamba , mkoa umepata Bilioni 8.440 za fedha za Uviko ambazo zilitumika kujenga vyumba vya madarasa,Mradi wa Sequip Bilioni 5.6 na kujenga shule 12 mpya za Sekondari ambapo kila shule ilitumia milioni 470 kila ujenzi.

By Jamhuri