Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Wakili na Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara wa Chama cha ACT -Wazalendo, Mwanaisha Mndeme, amejitosa kugombea Ubunge katika Jimbo la Kigamboni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea kiti hicho, Mwanaisha ambaye pia ni katibu wa Idara ya Mambo ya Nje, amesema, lengo la kugombea ni kuwasadia Wana Kigamboni kuwaletea maendeleo na kulinda thamani ya kura za wananchi wa jimbo lake zisipotee bure.
Amesema anaingia katika kinyang’anyiro hicho ,kwa nia moja ya kuwatumikia wananchi wa Kigamboni kwa moyo wa dhati ,uadilifu na bidii ambapo anaamini Jimbo hilo lina fursa kubwa za maendeleo ambazo zinahitaji kiongozi thabiti aliye karibu na wananchi anayesikiliza mahitaji yao.

Mwanaisha amesema jimbo hilo limekuwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo za miundombinu mibovu ya barabara katika kata tatu za Kimbiji, Pemba Mnazi na Kisarawe wakazi katika eneo hilo wamekuwa wakipata shida ya usafiri kufika katika maeneo yao ya kupata Riziki kwa hiyo atahakikisha anakuwa sauti yao katika upatikanaji wa barabara safi na salama Kwa wakazi hao,
Pia amesema atakuwa mwalikishi wa Wana Kigamboni ,katika upatikanaji wa vivuko vya uhakika na bure atahakikisha wanavuka bila malipo katika daraja la Mwalimu Nyerere kama ilivyo kwa Tanzanite kwani suala la mwananchi kuvuka salama ni la Serikali na haipaswi kukwepa jukumu la kutoa huduma ya kuvushwanaKigamboni kwasababu kwetu ni huduma ya lazima.
“Ama ACT- Wazalendo tumejiridhisha kuwa kususia uchaguzi ,utafurahiwa na CCM kwani tumeshuhudia uchaguzi wa marudiano Zanzibar wa mwaka 2015 baada ya CUF kususia CCM iliendelea bila kujali “amesema.

Amesema iwapo atapata ridhaa na chama chake pamoja na wanaKigamboni ,atahakikisha anatumia taaluma yake kuungana na wenzake kutunga Sheria zenye tija kwaWanakigamboni na Watanzania kwani shabaha za chama chake ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinamnufaisha kila mtu.
