Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Nachingwea

Wakulima wa zao la Korosho katika vijiji vya Kiparamtuwa na Farmseventine katika WIlaya ya Nachingwea mkoani Lindi wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya kilimo na Chakula kwa kuwapatia pembejeo za ruzuku aina ya Simba Sulphur Dust Dust kwa ajili ya kusaidia kupulizia kwenye mashamba yao ya korosho.

Wakizungumza na waandishi wa habari jna kwenye kijiji cha Palamtua, Noel Mmole mkazi wa kijiji cha Farm Seventeen na Mwanahamisi Rashidi mkazi wa Palamtua walisema kuwa dawa za ruzuku zinazotolewa kwa wakulima wa zao la korosho ni msaada mkubwa kwani Serikali inastahili kupewa pongezi za dhati.

Wakulima wadogo hao wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwasaidia wakulima wa zao la korosho ambalo ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa mikoa ya kusini pamoja na Serikali yenyewea.

Alisema wamefanikiwa kuchukuwa pembejeo aina ya Simba Sulphur Dust kwa ajili ya mashamba yao ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji na wao kujipatia kipato kitakacho wawezesha kumudu gharama za maisha yao ikiwemo kulipa ada za shule kwa watoto wao.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI Odas Mpunga alisema kuwa wamepewa pembejeo zaidi ya tani 3000 kwa wakulima wa zao la korosho ambazo zitakwenda kusaidia kuepuka mashamba hayo kukumbwa na wadudu waharibifu.

Pia ametoa viwatilifu zaidi ya lita milioni 16 kwa ajili ya kupulizia kwenye mashamba ya korosho na amewahamasisha wakulima wa zao hilo kuzitumia vizuri pembejeo za ruzuku walizopatiwa ili zikalete tija kwenye zao hilo na Serikali iweze kupata mapato zaidi baada ya mavuno.