Donald Trump ambaye amesema kwamba anajitolea kwenda nchini Uturuki kwa mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine ikiwa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin pia atajitokeza.
Rais wa Marekani Donald Trump ambaye anaendelea na ziara yake ya siku nne huko Mashariki ya Kati amesema leo kwamba anajitolea kwenda nchini Uturuki kwa mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukrsine ikiwa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin pia atajitokeza.
Trump amewaambia hayo waandishi wa habari wakati alipokuwa akisafiri kwa ndege kutoka Saudi Arabia kuelekea Qatar na ambapo amefanya mazungumzo na utawala nchini Qatar.
Alipoingia madarakani mwanzoni mwa mwaka huu, Trump aliahidi kuumaliza mzozo huo lakini mpaka sasa jitihada zake bado zimegonga mwamba na Urusi imepuuza mpango ulioungwa mkono na Ukrsine wa kusitisha mapigano kwa siku 30.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemrai rais Putin wa Urusi kwamba wakutane kwa mazungumzo ya moja kwa moja nchini Uturuki siku ya Alhamisi lakini hadi sasa Urusi bado haijathibitisha kwamba ni nani atakayehudhuria mkutano huo.
