RAIS Donald Trump wa Marekani ametangaza kuahirisha utozaji ushuru wa asilimia hamsini kwa bidhaa zinazotoka Umoja wa Ulaya uliokuwa uanze tarehe Mosi Juni.
Trump alisema sasa hatua hiyo itaanza kutekelezwa tarehe 9 Julai, na kwamba amechukuwa uamuzi huo ili kupisha majadiliano na Umoja wa Ulaya.
Makubaliano hayo yalifikiwa jana baada ya rais huyo wa Marekani kuzungumza na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ambaye alimuambia Trump kuwa Ulaya inataka kujadiliana kwa kina.
Rais huyo wa Marekani aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo hapo jana kwamba alishatowa kauli yake kwa kila aliyetaka kumsikiliza na kwamba sasa anatazamia pande hizo mbili zitakaa kitako haraka.
Trump alishatangaza kuiwekea Ulaya ushuru wa asilimia 50 akiituhumu kwa ukaidi.
