URUSI na Ukraine zimebadilishana mamia ya wafungwa ambayo ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya mpango huo uliashirikia hatua isio ya kawaida ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
Kando na hatua hiyo mataifa hayo yameshindwa kufikia makubaliano ya kusitisha vita vyao vilivyodumu miaka mitatu.
Saa chache kabla ya zoezi hilo kufanyika, mji wa Kyiv na maeneo mengine ya Ukraine yalipitia mashambulizi makali ya angani kutoka Urusi yaliyosababisha mauaji ya watu 12 huku wengine wakijeruhiwa.
Maafisa wa Ukraine wameyaelezea mashambulizi hayo kuwa mabaya na makubwa tangu Urusi ilipoivamia mnamo Februari 24 mwaka 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatolea mwito viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza shinikizo kwa Urusi kuachana na mashambulizi yake dhidi ya Ukraine na kupendekeza vikwazo zaidi kwa jirani yake huyo.
