📌REA yaeleza mchango wake katika kupunguza athari za uharibifu na uchafuzi wa mazingira.
📍Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kilele cha Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026 yanayofanyika jijini Dodoma.
Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi ametembelea banda la REA leo Juni 5, 2026 ambapo ameelezwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Wakala maeneo ya Vijijini na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala Mha. Advera Mwijage.
Halikadhalika, Mha. Mwijage amemueleza Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi kuwa, kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imesaidia kupunguza athari za uharibifu na uchafuzi wa mazingira.
Maonesho ya mwaka huu yamepambwa na kauli mbiu isemayo: Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania




