Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025. ujenzi wa Kiwanja hicho cha Msalato unahusisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway) jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na Miundombinu mengine.