Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kigoma

Chama cha ACT Wazalendo kimeahidi kukomesha changamoto ya migogoro ya ardhi endapo wananchi watakipa ridhaa ya kuongoza kwa kuchagua wabunge na madiwani wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Akifafanua wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika, Oktoba 07, 2025 katika kata ya Kitanga jimbo la Kasulu vijijini, kiongozi mstaafu wa chama hicho, Zitto Kabwe hatua hiyo itawapa sauti viongozi watakaotokana na chama hicho kusimama na kuwatetea wananchi.

Aidha, amesema wakati nchi inapata uhuru eneo la hifadhi lilikuwa ni asilimia 12 pekee ya huku idadi ya watu ikiwa ni 9 milioni, hali hiyo ni tofauti na sasa ambapo eneo la hifadhi ni asilimia 50 wakati idadi ya watu ni zaidi ya 60 milioni.

Ameongeza kuwa serikali inayoongozwa na chama cha CCM imekuwa ikichukua maeneo na kuyageuza kuwa hifadhi, huku ikiacha eneo dogo kwa wananchi kwa ajii ya shughuli za uzalishaji.

Naye mgombea ubunge wa jimbo la kasulu vijijini kwa tiketi ya chama hicho, Bigaye Enock ameahidi kuboresha huduma za afya katika jimbo hilo kwa kuhakikisha kinamama wajawazito hawatozwi gharama za vifaa wakati wa kujifungua katika jimbo hilo.