Rais wa Marekani Joe Biden anawaalika viongozi kuhudhuria mkutano kuhusu Ukraine nchini Ujerumani kuratibu juhudi za nchi zaidi ya 50 zinazoiunga mkono Ukraine katika kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Taarifa hiyo imetangazwa na Ikulu ya Marekani kwamba mkutano huo utafanyika mwezi ujao wa Oktoba. Katika taarifa yake Biden ametangaza msaada mpya wa thamani ya dola bilioni nane kabla kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mjini Washington.

Biden ataanza ziara ya siku tatu nchini Ujerumani kuanzia Oktoba 10. Atakutana na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, na Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir, mjini Berlin.

Baadaye ataitembelea kambi ya jeshi la anga la Marekani mjini Ramstein. 


 

Please follow and like us:
Pin Share