BOT: BENKI ZILIZOFUNGIWA ZITAKUWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU

Benki Kuu ya Tanzania(BOT) imezifutia leseni benki 5 baada ya kukosa mtaji na fedha za kutosha kujiendesha.

Benki hizo ni Covenant Bank for Women, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank, Meru Community Bank na Kagera Farmers’ Cooperative Bank.

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof Beno Ndulu amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya BOT kujiridhisha kuwa Benki hizo hazina mtaji wa kutosha kujiendesha kwa mujibu wa sharia za usajili wa taasisi hizo.

Kwa mujibu wa Prof Ndulu, Benki kuu imechukua hatua hiyo ili kulinda maslahi ya wateja wenye amana katika taasisi hizo kwani kuziruhusu kuendelea kutoa huduma kunaweza kukasababisha fedha za wateja kupotea.

Jumatano jioni benki kuu ya Tanzania imetangaza kuzifutia usajili na kuziweka chini ya uangalizi wa Bodi ya Bima na Amana Benki Tano zilizokuwa zikitoa huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini.