Rais Samia Suluhu Hassan amelitangazia taifa kifo cha Mzee Cleopa David Msuya, aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania na Waziri Mkuu kilichotokea leo Mei 7, 2025 majira ya saa tatu asubuhi, katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam alipokuwa amelezwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Taarifa zaidi ua mipango kamili ya msiba itaedelea.
Rais Dk Samia ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia Mei 7 hadi 13, 2025.
Rais Dk Samia anawapa pole ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa msiba huu.
