Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepanga kupokea Maoni ya Wadau  kuhusu Bunge kuridhia Mkataba wa Umoja wa Afrika kuhusu Usalama wa Mtandao na Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2014 [The African Union Convention on Cyber Security and Personal Data Protection, 2014]. 

Mkutano wa kusikiliza na kupokea maoni ya wadau kuhusu Bunge kuridhia Mkataba huo utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 26 Oktoba, 2026 kuanzia saa 4:00 asubuhi, katika Ukumbi Na. 231 uliopo ghorofa ya 2 katika Jengo la Utawala.

Kwa kuzingatia umuhimu wa ushiriki wa wananchi, Kamati inawaalika watu wenye maoni kufika katika Mkutano huo na kuwasilisha maoni yao kabla ya Azimio kupelekwa katika hatua nyingine.

Aidha, maoni yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya posta kupitia anuani ya Ofisi ya Bunge au kupitia barua pepe ya [email protected] au [email protected]

Mkataba husika unapatikana katika tovuti ya Bunge kupitia https://www.parliament.go.tz/documents/resolutions