Category: Kimataifa
Ukraine yailenga miundombinu ya Urusi kwa kutumia dronI
UKRAINE kwa mara nyingine imefanya mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani kwenye mikoa ya Urusi Mashambulizi hayo ya usiku kucha wa kuamkia siku ya Jumamosi yamesababisha milipuko katika miundombinu ya kuchakata mafuta. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema hii…
Marekani, Umoja wa Ulaya zafikia makubaliano ya ushuru
Marekani na Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano ya kibiashara yanayoshusha ushuru kwa bidhaa za Ulaya hadi asilimia 15 kutoka kitisho cha awali cha Rais Donald Trump cha asilimia 30. Trump na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen,…
Urusi yaimiminia tena Ukraine ‘mvua ya droni’
Jeshi nchini Ukraine liliwasha ving’ora vya tahadhari kwenye maeneo mengi ya nchi hiyo kufuatia mashambulizi mengine makubwa ya droni kutoka Urusi usiku wa kuamkia Jumatatu (Julai 28). Kwa mujibu wa jeshi, wakaazi wa mji mkuu, Kiev, na maeneo mengine walitakiwa…
Papa Leo aonya kuhusu ‘matumizi ya nguvu kiholela’ huko Gaza
Papa Leo alionya dhidi ya “matumizi ya nguvu kiholela” na “uhamisho wa kulazimishwa wa watu” wa Gaza katika mazungumzo ya simu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas siku ya Jumatatu, kulingana na taarifa kutoka Vatican. Papa pia alisisitiza haja ya…
Waziri wa Cuba ajiuzulu baada ya kusema nchi haina ombaomba
Waziri wa Kazi wa Cuba Marta Elena Feitó Cabrera amelazimika kujiuzulu baada ya kutoa maoni ya kukanusha kuwepo kwa ombaomba katika kisiwa hicho kinachoongozwa na Wakomunisti. Waziri alikuwa amesema hakuna kitu kama “ombaomba” nchini Cuba na watu wanaopitia takataka walikuwa,…
China yaiunga mkono Iran dhidi ya uonevu
China itaendelea kuiunga mkono Iran katika kulinda mamlaka yake ya kitaifa na heshima, pamoja na kupinga siasa za ukuu na uonevu. Haya yamesemwa leo na waziri wa mambo ya nje wa China kwa mwenzake wa Iran. Katika taarifa iliyotolewa na…





