JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Kitaifa

Singasinga ‘anyooka’

Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashitaka 12 ya uhujumu uchumi, ikiwamo kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani  22, 198,544.60 na…

Ardhi Temeke kikwazo

Zaidi ya kesi 100 za migogoro ya ardhi zimekwama kutolewa hukumu katika Baraza la Ardhi Wilaya ya Temeke kwa sababu ya kukosa printer na vifaa vingine muhimu. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, mmoja wa walalamikaji hao, Aidan Amon, ambaye ni miongoni mwa…

‘Ukipita mwendokasi jela’

Wewe ni dereva? Umewahi kuendesha gari lako binafsi au pikipiki kwenye barabara ya mwendokasi? Sasa Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limeanza kufanya operesheni ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wote wanaokiuka taratibu. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, Kamanda wa…

Profesa Tibaijuka atema mil. 1,600/- za Rugemalira

Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (69), yuko tayari kurejesha Sh bilioni 1.6 alizopewa na James Rugemalira ili zimsaidie mfanyabiashara huyo atoke rumande. Profesa Tibaijuka alikuwa miongoni mwa wanufaika wa mabilioni ya shilingi ‘yaliyomwagwa’ na Rugemalira aliyezipata kutoka kwenye…

DED amaliza mgogoro wa ardhi Pugu

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, ametoa uamuzi juu ya mgogoro wa ardhi unaoendelea katika eneo la Pugu Bombani, Dar es Salaam na kuwapa ushindi wafanyabiashara ndogo ndogo. Mkurugenzi Shauri ameliambia JAMHURI kuwa mgogoro huo tayari wameumaliza na eneo…

Kesi ya Luwongo wiki ijayo

Kesi inayomkabili mfanyabiashara, Khamis Said, maarufu Meshack (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe, Naomi Marijani, imepigwa tarehe hadi Oktoba 7, mwaka huu kutokana na kutokamilika kwa upelelezi.  Wakili Mwandamizi wa Serikali, Wankyo Simon, amemweleza Hakimu Mkazi, Salum Ally, mbele ya mahakama kuwa…