Category: Kitaifa
Waasi M23 wachapwa Goma
Brigedi ya Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) inayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, imewadhibiti waasi wa kundi la March 23 (M23). Brigedi hiyo inayojulikana kwa kifupi kama FIB, inaongozwa na Mtanzania, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa. Kwa sasa imelidhibiti eneo la Goma.
Edwin Butcher: Hatuhusiani na Dk. Amani
Mmiliki wa duka la nyama linaloitwa Edwin Butcher la Rwamishenye, Bukoba, amejitokeza na kusema kuwa bucha yake haina uhusiano wowote na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Bukoba, Dk. Anatory Amani, au udini kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.
Mapapa wa ‘unga’ watajwa
*Kinondoni, Magomeni, Mbezi, Tanga watia fora
*Wamo Wakenya, Wanigeria, waimba taarab Dar
*Wengine wapata dhamana kimizengwe, watoroka
Vita dhidi ya wauzaji na wasafirishaji dawa za kulevya inazidi kupamba moto, na sasa JAMHURI imepata orodha ya watu wengine 245 wanaotajwa kuwa ndiyo ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu hapa nchini.
Mtendaji mkuu Osha alalamikiwa Tughe
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, amelalamikiwa mbele ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), kuwa anawaongoza kimabavu wafanyakazi wa taasisi hiyo ya Serikali.
BRN kuinua elimu nchini
Kiwango cha elimu Tanzania kinatarajiwa kupanda, baada ya Serikali kuzindua mpango wa kufanikisha Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN).
Wauza unga 250 nchini watajwa
*Soma orodha uone maajabu, wamo masheikh, wachungaji
*Wengi wanatoka Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, Morogoro
*Mahakama yawaweka chini ya uangalizi, wanaripoti polisi
Majina ya Watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamejulikana, na JAMHURI imeamua kuyachapisha. Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wamo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada, huku wengine wakijifanya ni wazee wa kanisa na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.