Category: Kitaifa
PPF yafafanua michango ya zamani
Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) umewatoa wasiwasi wafanyakazi wa mashirika ya umma waliochangia tangu mwaka 1978, kwa michango isiyoonekana kwenye mtandao wa mfuko huo.
TEF, MCT wampongeza Kikwete
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua ya kutangaza akiwa jijini London kuwa kuanzia mwakani, Serikali itatunga Sheria ya Haki ya Kupata Habari.
Chadema ‘Kimewaka’
Chimbuko migogoro ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unasababishwa migongano wa kupata madaraka ndani ya chama hicho, JAMHURI limebaini
Imelezwa kuwa mtafaruku uliotokea mwishoni mwa wiki na kusababisha kusimamishwa kwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha wa Chadema kwa muda usiojulikana ni mgongano wa kutafuta madaraka ndani ya chama hicho.
‘Majangili’ 20 hatari
- JWTZ watisha, maofisa Maliasili 16 wakamatwa
- Mmoja akutwa anamiliki bunduki 5 za rifle kali
- Mbunge Mtutura ahojiwa, Nchambi naye atajwa
- RCO aliahidiwa dola 3,000 akawaachia Waarabu
Operesheni Tokomeza inayoendeshwa chini ya usimamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imewakamata watumishi kadhaa wa Serikali wanaotuhumiwa kujihusisha na ujangili. Operesheni hiyo inaongozwa na Luteni Kanali A. Sibuti.
Rushwa yazigonganisha Mahakama, Wizara
Wizara ya Nishati na Madini imeingia kwenye mvutano na Mahakama baada ya mhimili huo kuamuru raia wa China aliyekamatwa akitorosha madini ya tanzanite, arejeshewe madini hayo kinyume cha sheria.
Maswi: Kila Mtanzania atapata umeme
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imesema umeme ni huduma ya lazima kwa Watanzania na itafanya kila liwalo kuhakikisha kila Mtanzania anapata umeme. Msimamo wa Serikali umetolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, wakati akizungumza katika kipindi cha Tuambie kupitia runinga ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wiki iliyopita.