Category: Kitaifa
Vita kubwa TANESCO
*Wabunge wajiandaa kukwamisha tena bajeti ya Wizara ya Nishati, wahoji zabuni ya mafuta BP
*Wajiandaa kuwang’oa Waziri Profesa Muhongo, Katibu Mkuu Maswi Ijumaa ya wiki hii
*Katibu Mkuu aanika ukweli, asema Wizara yake haikufanya manunuzi waliohusika ni RITA, Zitto anena
[caption id="attachment_219" align="alignleft" width="243"]Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo[/caption]Kuna kila dalili kuwa imeibuka vita ya wazi kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, William Mhando, akipigiwa debe la wazi na wabunge.
Taarifa zilizopatikana kwenye ofisi za Bunge zinasema kuwa Kamati ya Nishati na Madini inajipanga kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, Injinia Mhando, hatarejeshwa kazini huku wizara ikisisitiza kuwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wala hajafukuzwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, naye ana msimamo kuwa Mhando ameonewa na wizara inaweza kujiokoa kwa kumrejesha ofisini kisha ufanywe uchunguzi maalumu utakaoendeshwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Ufisadi watikisa Bunge
*Unahusu kada wa CCM anayechimba urani
*Profesa Tibaijuka amtwika mzigo Jaji Werema
*Naibu Spika aagiza Waziri Muhongo ajiandae
*Sinema nzima imeibuliwa na Halima Mdee
Wafanyabiashara ndugu wanaodaiwa kubadili matumizi ya ardhi kutoka uwindaji wa kitalii na kuanza harakati za uchimbaji madini ya urani, wameibua mgongano mkubwa bungeni na serikalini. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amemwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, asaidie kupata utatuzi kashfa hiyo.
Hotuba ya Lissu iliyolitikisa Bunge, Serikali
*Atoboa siri majaji wengi ‘vihiyo’, washindwa kuandika hukumu
*Aeleza namna wakuu wa wilaya walivyoteuliwa kwa rushwa
*Yumo mwingine aliyehukumiwa kwa ubaguzi wa ukabila
Ifuatayo ni sehemu ya maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, kuhusu Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013. Lissu alitoa maoni haya na kwa kiasi fulani yaliibua mjadala mkali bungeni, huku Serikali ikitaka aondoe baadhi ya maneno, na yeye akakataa. Endelea…
UTEUZI WA MAJAJI
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua ukweli kwamba Rais Kikwete ameteua majaji wengi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kuliko marais wengine wote waliomtangulia kwa ujumla wao. Rekodi hii peke yake inaonyesha kwamba Rais anatambua umuhimu wa Mahakama Kuu kuwa na watendaji wa kutosha wa utoaji haki ili kutekeleza dira ya ‘haki kwa wote na kwa wakati.’
‘Majaji ndiyo waliomtuma Lissu’
Hotuba kali ya Tundu Lissu ya kukosoa uteuzi wa majaji dhaifu uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete, imeelezwa kwamba ina baraka zote za baadhi ya viongozi waandamizi wa Mhimili wa Mahakama, JAMHURI limeelezwa.
HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
DIRA YA WIZARA:
Kuwa na uhakika wa milki za ardhi, nyumba bora na makazi endelevu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
DHIMA:
Kuweka mazingira yanayofaa kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma za ardhi, nyumba na makazi
- TAKUKURU Lindi yajiimarisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu thamani ya kura
- ‘Wanaodai utaratibu wa kumpata mgombea urais CCM haukufuata wanajitoa ufahamu’
- Othman : Viongozi wa dini wana haki haki ya kuangalia haki, amani na utulivu
- Singapore na Tanzania zakubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi
- Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya CCM
Habari mpya
- TAKUKURU Lindi yajiimarisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu thamani ya kura
- ‘Wanaodai utaratibu wa kumpata mgombea urais CCM haukufuata wanajitoa ufahamu’
- Othman : Viongozi wa dini wana haki haki ya kuangalia haki, amani na utulivu
- Singapore na Tanzania zakubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi
- Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya CCM
- Samia amkabidhi mgombea mwenza Nchimbi ilani ya CCM
- INEC yaondoa fomu za uteuzi wa Wagombea urais
- Rais Samia amewasha umeme vijiji vyote Arusha
- TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga
- Global Education Link yaanza kusafirisha wanafunzi nje ya nchi
- Viongozi, wasanii na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni za CCM
- Shamrashamra za uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu CCM
- Mgombea nafasi ya urais CCM akiwasili viwanja vya Tanganyika Packers
- Kitila Mkumbo, Angellah Kairuki warudisha fomu kwa mtindo huu
- Watoto wawili wauawa kwa risasi kanisani Marekani
Copyright 2024