Category: Siasa
Tumekubali kuwa punda wa Wakenya
Biashara zinahitaji akili za kisasa
Wiki mbili zilizopita, nilipata wasaa wa kuongea kwa kirefu kwa njia ya simu na mjasiriamali kutoka mkoani Singida. Katika mazungumzo yetu mjasiriamali huyu wa miaka mingi alilalamika namna biashara zilivyobadilika nyakati hizi na namna ushindani unavyotishia mustakabali wake.
Mjasiriamali huyu alinipa mifano ya namna zamani alivyokuwa akipata faida kubwa katika bidhaa mbalimbali. Anaeleza, “Zamani nilikuwa nakwenda Dar es Salaam na kununua unga wa ngano kwenye mifuko ya kilo 50, nikija hapa Singida nikiuza kwa jumla ninapata faida ya hadi shilingi elfu tano. Leo hii mfuko wa unga wa kilo 50 huwezi amini, ninapata faida isiyozidi shilingi mia tano!
KAGAME NI MTIHANI
Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa uangalifu
Kama kuna nchi ambayo imeweza kurithi vilivyo udanganyifu wa kisiasa na unafiki ambavyo himaya kuu ya zamani ya ‘Roma’ ilikuwa navyo, basi ni Taifa kubwa la sasa ‘Marekani’.
Hakika Marekani ndiyo dola kubwa linaloongoza kwa kuwa ‘wakili wa shetani (the devil’s advocate)’.
Katika enzi hizi za Marekani kuwa dola kubwa, yaani kuwa babeli mkuu, damu ya watu wasio na hatia na wasioujua hata huo ubepari wenyewe imemwagika mno na hakuna hata chembe ya soni au hatia ambayo Marekani imejivisha. Hakika imekuwa Roma. Roma ya ustaarabu na sheria vilivyoleta mateso yasiyomithilika.
Kwanini Zanzibar?
Hili ni swali linalogonga vichwa vya wananchi wengi siku hizi. Hivi karibuni kule bungeni Dodoma kulitokea kadhia kubwa iliyosababisha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kususia vikao na kutoka nje ya bunge hili.
Tangu lini wapinzani wanawapenda wananchi?
Vyama vya upinzani vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika Bunge Maalum la Katiba vimesusia vikao vya bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu.
Wapinzani wametoa sababu zao za kuchukua hatua hiyo. Kwa mfano, wamesema Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, wametoa vitisho kwamba kukiwapo Serikali tatu Jeshi litachukua nchi.
Vituko vya DC Geita vyaongezeka – 3
DC adaiwa kumtisha Roboyanke
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyara, Makoye Roboyanke (CCM), ambaye inadaiwa alivuliwa madaraka hayo na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie, amedai kuwa Septemba 10, 2013 mchana akiwa shambani kwake kijijini hapo, alipokea simu ya vitisho kutoka kwa kiongozi huyo wa Serikali.
“Alijitambulisha kwa jina moja la Mangochie na kwamba ndiye Mkuu wa Wilaya ya Geita, akaniuliza jina langu nami nikamjibu… akaniuliza ninachofanya kwa wakati huo na kazi yangu hasa ni nini, nikamwomba arekebishe kauli, na baada ya kurekebisha kauli na kuniuliza maswali ya msingi nilimpa ushirikiano.
Habari mpya
- Ujifadhi ndio moyo katika sekta ya utalii – Kamishna Badru
- Dk Tulia kujitoa kinyang’anyiro cha uspika kwazua mjadala
- Dk Tulia ajiondoa kugombea uspika
- ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya uchaguzi mkuu
- Rais Mwinyi aagiza kuendeleza amani kwa maendeleo ya nchi
- Serikali yatoa milioni 403/- kurejesha mawasiliano Mbinga
- Ujenzi soko la majengo kukamilika Desemba mwaka huu – RC Senyamule
- RC Makala asisitiza kulinda amani mpaka wa Namanga
- Rais Mwinyi ateua wajumbe wa Baraza ka Wawakilishi
- Mawakili wa Serikali wampongeza Mwanasheria Mkuu Johari
- Maonesho ya kilimomisitu kufanyika Musoma Novemba 13 na 15, 2025
- Kauli ya Rais Samia imetupa utulivu kuendelea na majukumu – Wananchi
- Rais Dk Samia apokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi
- Mwenyekiti ACT- Wazalendo aanza ziara ya maalum kukutana na wanachama Pemba
- Rais Dk Mwinyi amuapisha mwanasheria mkuu wa Z’bar