Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Bunda


*Chasisitiza wajumbe wa mwaka
2022 ndiyo wapiga kura

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bunda mkoani Mara, kimesema wajumbe waliochaguliwa mwaka 2022 ndiyo watakaoruhusiwa kupiga za maoni za kuchagua mbunge na si vingenevyo.

Kauli ya chama hicho imekuja siku chache baada ya taarifa za kupotosha kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu ambao wanaonekana kuanza kujipitisha ndani ya jimbo hilo wakisema kuna wajumbe wapya wameongezwa.

Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda, Michael Chonya amesema wajumbe hao ndiyo wanaruhusiwa kisheria baada ya chama hicho kufanya mabadiliko ya Katiba mwaka huu jijini Dodoma na hakuna wajumbe wapya waliongezwa.

Kumekuwapo na taarifa za upotishaji mkubwa kuwa kuna wajumbe wameongezwa kwa ajili ya kupiga kura za maoni wakati wa uchaguzi wa ubunge, hakuna kitu kama hicho, chama kiko makini kinafuatilia mwenendo wote.

Katika siku za karibuni kumekuwa na uvumi wa habari kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna wajumbe wapya wameongezwa, hakuna kitu kama hiki, napenda kusisitiza hili kuwa wajumbe ambao wa haki ya kupiga kura ni wale ambao walichaguliwa mwaka 2022 tu.

Uchaguzi wa chama chetu unaendeshwa kwa kanuni na zinaelekeza wapiga wa kura za maoni ni wale waliochaguliwa mwaka 2022 tu, hivyo chama hakitamfumbia macho mtu au kikundi cha watu kinachokusudia kuvunja taratibu na kanuni zetu,wapiga kura halali ni hao na si vinginevyo.

Anasema katika siku za karibuni kuna baadhi ya watia nia watatu ambao hakuwataja majina, wamekuwa wakipita kwenye matawi mbalimbali jimboni humo kwa ajili ya kuzungumza na wajumbe, jambo ambalo halikubaliki kufanya hivyo kwa sababu muda haujafika.

Wapo baadhi ya watia nia ambao wanapita kwenye matawi mbalimbali na kutengeneza wajumbe wa mchongo, tumekuwa na kazi ya kuwaondoa na kurudisha wajumbe halali waliochaguliwa mwaka 2022.

Hawa watu walikuwa wanatumia makatibu wa matawi na kata kutengeneza wajumbe feki, mimi nimezunguka kote huko, nimemaliza ziara yangu juzi nikawafute wote wa mchongo nikarejeshe wa zamani kwa maana hao waliotengezwa wapya kwa ajili ya wagombea tumefuta,anasema.

Anasema kitendo cha kuwafuta kinaonekana kuwachukiza kwa sababu ameharibu mfumo wao na kutoa maelekezo kwa makatibu wote wa matawi kuwa ni marufuku kuingia mtu yeyote mpya.

Kitendo hiki kimeonekana kuwachukiza kwa sababu nimevunja mtandao wao, nimetoa maelekezo kwa makatibu wa matawi wote kuwa ni marufuku kuingiza mtu yeyote mpya, ni marufuku maana uchaguzi wa wajumbe ulifashafanyika mwaka 2022.

Siku zote tinafauata maelekezo ya chama kama nafasi ikiwa inatakiwa kubaki wazi mpaka uchaguzi upite kwa sababu kufanya uchaguzi tunazalisha makundi mengine ndani ya chama kabla hatujaenda kwenye uchaguzi wa kura za maoni, hapa kunakuwa na makundi ya aina mbili ka hiyo nilitoa hayo maelekezo na kufuta wale wajumbe wote ambao wametengenezwa kwa ajili ya maslahi ya watu,anasema.

Anasema wajumbe wa Jimbo la Bunda Vijijini linakadiriwa kuwa na wajumbe karibu 6,300 hivi, lakini wapo walipachikwa katika maeneo tofauti tofauti kama Kata ya Unyari na Nyamuswa.

“Tumefanya kazi kubwa sana ya kubaini wajumbe feki katika kata za Unyari na Nyamuswa, hawa watu wameangalia zile center kubwa kubwa ambazo zina watu wengi, kwa sababu taarifa za uchaguzi wa mwaka 2022 ziko ofisini, niliamua kwenda na orodha ile ile ilinisaidia sana nilivyofika nikakuta kuna watu wapya nikawa na kazi ya kufuta wote na kuwaeleza viongozi jamani hawa wajumbe wa zamani ndiyo halali kwanini mmeonewa watu hivi? Watu hawa walichaguliwa vizuri.

Moja kwa moja hapa niligusa maslahi yao kwa sababu wametumia nguvu kubwa kutengeneza wajumbe feki baada ua Mkutano Mkuu kupitisha Katiba mpya kwamba wajumbe watakao piga kura ni watu fulani,anasema.

Anasema kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwa makatibu wa kata ambao ni watu anafanya kazi siku zote na kuwapa maelekezo juu ya shughuli za chama.


Siku zote napopokea maelekezo kutoka mkoani nawaita wote kuwapa maelekezo wakafanyie kazi, huo ndo utaratibu, kukutana na mimi na makatibu wangu ni lazima hata katibu mkuu akitaka kufanya jambo lake anawaita makatibu wa mikoa wanakaa wanajadiliana.

Kwa mfano pale Nyamswa mwanzoni kulikuwa na malalamiko mengi juu ya kiongozi fulani aliyeko madakarani ametengeneza wajumbe kupitia kwa katibu kata, huwa nawaita kwa ajili ya kushughulikia kasoro hizi zinazojitokeza.


Kuna mgombea alikodi gari na kuwapeleka Musoma baada ya kuona sisi tumemaliza kazi ya uhakiki ili waka-riot kule, na katibu wa mkoa akaeleza, juzi nimetoka huko kukutana na halmashauri kuu ya tawi, mwisho wa siku yule mwenyekiti wa tawi aliyebeba wale wajumbe aliomba msamaha kwenye kikao, kwa mtu anayefoji watu atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni za chama kwa kufikishwa kwenye tawi,kata,tarafa,wilaya hadi mkoa,anasema.

Anasema wajumbe wengi kwenye kikao walionekana kunyosheana kidole kwa kusema jamani malenge yatatuua. Melenge ni lugha inayotumiwa na wajumbe wapokea fedha za watia nia.

Jamani mélange itatuua tutagombana sana hatutaachwa salama kwenye mkutano huo, lazima tuwe makini,anasema.