Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha

Chama cha waongoza watalii Tanzania (TTGA) wameiomba serikali iweze kuwatambua kisheria ili waweze kulipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria kwani hiyo ni taasisi kamili iliyokamilika .

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa TTGA Robert Marks wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa 26 wa chama hicho uliofanyika.mkoani Arusha .

Marks amesema kuwa, endapo serikali itawatambua kisheria wataingizwa kwenye Sheria na kuweza kutungiwa Sheria zao zitakazowaongoza sambamba na kulipwa stahiki zao zote ipasavyo .

Amefafanua kuwa, kuna zaidi ya waongoza watalii elfu moja nchi nzima ambapo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa huduma za afya kutokana na kutokuwa na bima ya afya hivyo kuomba serikali kuwaangalia kwa jicho la pili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TATO Wilbar Chambulo amesema kuwa ,waongoza watalii wanakabiliwa na changamoto nyingi saba hali.ambayo inapelekea wengi wao kutokuwa waaminifu kutoka na kiwango kidpgo cha mshahara wanacholipwa.

Chambulo amesema kuwa ,asilimia kubwa ya waongoza watalii hawawekewi NSSF zao jambo ambalo ni changamoto na wanaishia kulipwa mishahara kidogo kwani ajira zimekuwa hadimu .

“Tunaomba sana kwenye mitaala ya shule somo la “Tourguide “liingizwe kwenye mitaala ya shule kwani asilimia kubwa yao hawajui na hawajafundishwa hivyo likiwema mashuleni itasaidia sana wanapokuja kusomea wanakuwa na uelewa mkubwa sana .”amesema .

“Tunaomba sana serikali tutambuliwe kisheria kwani tukitambuliwa kwenye utaratibu wa kisheria tutalipwa vizuri na sio kuwa omba omba kwani mishahara yao ni midogo sana na hazitoshi kabisa kwani kima cha chini wanacholipwa ni 160,000 hela ndogo sana sisi tunataka kima cha chini kiwe 500,000 .”amesema Chambulo.

Naye Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori Dkt.Alexander Lobora ambaye alimwakilisha Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt Pindi Chana amewataka waongoza watalii hao kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kuhakikisha wanautangaza utalii popote watakapokuwa kwani wao ndio mabalozi wazuri ambao wanatakiwa wawakilishe nchi vyema kwani muda wote wapo na wageni hao.

Kwa upande wake Kamishna msaidizi kitengo cha maendeleo ya biashara Tanapa ,Jully Lyimo amesema kuwa, waongoza utalii ni mabalozi wazuri ambao wanaiwakilisha nchi ipasavyo hivyo amewataka kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwani huduma nzuri ndo itakayouza utalii wetu kwa wageni hao.

“Mtakapotoa huduma nzuri popote mmeiwakilisha nchi na hakikisheni mnajifunza kila kitu kipya duniani ili muweze kwenda na mabadiliko ya teknolojia yaliyopo sasa hivi.”amesema Jully.