𝙒𝙖𝙣𝙖𝙣𝙘𝙝𝙞 𝙬𝙖 𝙉𝙮𝙖𝙬𝙞𝙡𝙞𝙢𝙞𝙡𝙬𝙖 𝙟𝙞𝙢𝙗𝙤𝙣𝙞 𝙂𝙚𝙞𝙩𝙖 𝙬𝙖𝙢𝙚𝙢𝙥𝙤𝙠𝙚𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙨𝙝𝙖𝙣𝙜𝙬𝙚.

𝘼𝙩𝙤𝙖 𝙨𝙖𝙡𝙖𝙢𝙪 𝙯𝙖 𝙪𝙥𝙚𝙣𝙙𝙤 𝙣𝙖 𝙪𝙟𝙞𝙤 𝙬𝙖 𝘿𝙠𝙩. 𝙎𝙖𝙢𝙞𝙖.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amewasili na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Jumuiya, Viongozi mbalimbali wa Dini na maelfu ya wananchi wa Nyawilimilwa wilayani Geita kwa ujumla wake.

Pamoja na kuwasili kwake, Dkt. Migiro amepata wasaa wa kusalimiana na kuteta kidogo na baadhi ya kundi la watu wenye ulemavu ambapo wamempa salamu zao za shukrani kwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 kwa namna ambavyo serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita ilivyowagusa walemavu moja kwa moja katika kuwawezesha kiuchumi na kuwawekea mazingira bora na rafiki katika upatikanaji wa huduma za kiafya na kumuahidi kuwa wataendelea kuhamasishina na kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu kwa kwenda kumpigia kura Dkt. Samia, Wabunge na Madiwani wanaotokana na CCM.

Aidha, Dkt. Migiro ametanguliza salamu za ujio wa Dkt. Samia katika kunadi ilani ya CCM (2025/30) Sera na Ahadi zake kwa wananchi hao huku akiwasisitizia wananchi hao kuendelea kuwa na imani na CCM na kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29.