๐๐๐ฃ๐๐ฃ๐๐๐ ๐ฌ๐ ๐๐ฎ๐๐ฌ๐๐ก๐๐ข๐๐ก๐ฌ๐ ๐๐๐ข๐๐ค๐ฃ๐ ๐๐๐๐ฉ๐ ๐ฌ๐๐ข๐๐ข๐ฅ๐ค๐ ๐๐ ๐ ๐ฌ๐ ๐จ๐๐๐ฃ๐๐ฌ๐.
๐ผ๐ฉ๐ค๐ ๐จ๐๐ก๐๐ข๐ช ๐ฏ๐ ๐ช๐ฅ๐๐ฃ๐๐ค ๐ฃ๐ ๐ช๐๐๐ค ๐ฌ๐ ๐ฟ๐ ๐ฉ. ๐๐๐ข๐๐.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amewasili na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Jumuiya, Viongozi mbalimbali wa Dini na maelfu ya wananchi wa Nyawilimilwa wilayani Geita kwa ujumla wake.
Pamoja na kuwasili kwake, Dkt. Migiro amepata wasaa wa kusalimiana na kuteta kidogo na baadhi ya kundi la watu wenye ulemavu ambapo wamempa salamu zao za shukrani kwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป kwa namna ambavyo serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita ilivyowagusa walemavu moja kwa moja katika kuwawezesha kiuchumi na kuwawekea mazingira bora na rafiki katika upatikanaji wa huduma za kiafya na kumuahidi kuwa wataendelea kuhamasishina na kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu kwa kwenda kumpigia kura Dkt. Samia, Wabunge na Madiwani wanaotokana na CCM.
Aidha, Dkt. Migiro ametanguliza salamu za ujio wa Dkt. Samia katika kunadi ilani ya CCM (2025/30) Sera na Ahadi zake kwa wananchi hao huku akiwasisitizia wananchi hao kuendelea kuwa na imani na CCM na kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29.









