Na Manka Damian ,JamhuriMedia , Mbeya

NAIBU Waziri Mkuu ,Dkt.Dotto Biteko amesema kuwa amefurahishwa kuona mwitikio mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya katika mashindano ya Riadha Mbeya BETIKA Tulia Marathoni ikiwa ni msimu wa tisa .

Dkt.Biteko amesema hayo Mei ,10 2025 Jijini Mbeya wakati wa kuhitimisha mashindano ya Riadha Mbeya Betika Tulia Marathoni yaliyoshirikisha watu Mbalimbali kutoka maeneo mbali mbali hapa nchini .

“Leo wana Mbeya nimefarijika sana kushuhudia mwitikio huu mkubwa wa watu mmejaa kila mahali,mwaka 2024,idadi ya washiriki ilikuwa 1,760 tumeambiwa mwaka huu idadi ya washiriki imefika 2000 hili ni ongozeko la asilimia 13 mwamko huu ni uthibitisho na upendo mlio nao wananchi wa Mbeya kwa Dkt Tulia kwa kushiriki kuonyesha mpo na hamasa ya juu katika kuimarisha afya zenu “amesema Naibu Waziri Mkuu.

Hata hivyo Dkt.Biteko amesema kuwa waliobahatika kufanya kazi na Dkt .Tulia hawamchukulii kama Mbunge wa Mbeya ama Spika bali wanamchukulia mtu anayebuni vitu na vikatokea na kusema kuwa wakati anaanzisha Marathoni yawezekana kuna watu walibeza lakini kupitia marathoni ameweza kuwaunganisha wana Mbeya na kuwaunganisha kwa pamoja wajasiliamali.

“Leo hii ulizeni ni jinsi gani wafanyabiashara wanafanya biashara kupitia Marathoni ,amewaka pamoja wafanyabiashara, ameunganisha wanambeya hawazungumzi tena biashara ,wewe umekua Mwalimu wa wengi nakupongeza sanaa Sanaa kwa ubunifu huu mkubwa “amesema Dkt.Tulia.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa nyumba ambazo Dkt.Tulia amekua akijenga kwa wahitaji amesema kuwa jambo analolifanya kwa wahitaji la kuwajengea nyumba ni jambo la ibada .

Kwa upande wake Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini (IPU) amesema kuwa lengo mashindano hayo ni kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika sekta ya afya ,Elimu.

Dkt.Tullia amesema kuwa . mashindano hayo ni msimu tisa ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ambapo fedha zinazopatikana huenda kwenye miundo ya afya na elimu .

Amosi Juma ni mkazi wa Ilomba Jijini Mbeya amesema mashindano ya Riadha yameleta fursa kubwa kwa wafanyabiashara Jijini ambapo asilimia Kubwa ya wajasiliamali vipato vyao vimekuwa vikubwa kupitia mashindano hayo.

“Uwepo wa mashindano haya kwetu sisi wajasiliamali tulitamani hata yawekwe hata siku tano ,mwakani tena tunamwombea Mbunge wetu alete mashindano haya maana wengi kupitia mashindano haya biashara zetu zinasonga mbele na tunakua na uhakika wa kufanya biashara”amesema Juma.