Na Isri Mohamed, Jamhuri Media, Dar es Salaam

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 27, akiwa nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa shirika la afya duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt Faustine Ndugulile, kwa niaba ya wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na watanzania wote kwa ujumla, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi”

“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa, Bwana ametoa na bwana ametwaa apumzike kwa amani”