Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpa zawadi mwananchi aliyefika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa moyo ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha siku ya moyo duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 Septemba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpa zawadi mtoto aliyelazwa katika wodi ya wagonjwa maalumu (VIP Ward) ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha siku ya moyo duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 Septemba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpa zawadi mwananchi aliyefika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha siku ya moyo duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 Septemba.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akimkabidhi zawadi ya chakula mama wa mtoto aliyelazwa katika hospitali hiyo ikiwa ni muendelezo wa kuadhisha siku ya moyo duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 Septemba.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwakabidhi chakula ndugu wa mgonjwa aliyelazwa katika hospitali hiyo ikiwa ni muendelezo wa kuadhisha siku ya moyo duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 Septemba.

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Nuru Letara akimpa zawadi mzazi wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha siku ya moyo duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 Septemba.

 Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Mainda Hamu akimpa zawadi mzazi wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha siku ya moyo duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 29 Septemba.

*************************

Wajawazito wametakiwa kula vyakula bora na kuacha uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito ili waweze kujifungua watoto wenye afya bora .

Rai hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati akigawa zawadi kwa watoto wenye matatizo ya moyo wanaotibiwa katika taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es salaam.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema moja ya sababu zinazopelekea mtoto kuzaliwa na magonjwa ya moyo ni uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito.

“Ni vyema kina mama wajawazito wakajikinga na magonjwa ya moyo na kuepuka kufanya vitu ambavyo vitapelekea kuzaa mtoto mwenye matatizo ya moyo hii ikiwa ni pamoja na kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe”,.

 “Nawasihi wazazi kuleni vyakula bora ikiwa ni pamoja na  mboga za majani na matunda,  fanyeni mazoezi  ili kupunguza uzito mkubwa kwani uzito mkubwa unaweza kukupelekea kujifungua mtoto mwenye kisukari na ugonjwa huu unaweza  kusababisha mtoto kupata magonjwa ya moyo” , alisema  Dkt. Kisenge.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto na Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Sulende Kubhoja  alisema kumekuwa na dhana katika jamii kuhusu magonjwa ya moyo ni kwa watu wazima tu lakini siyo kweli kwani magonjwa hayo yanawapata hata watoto wadogo.

“Jamii inatakiwa kufahamu kuwa hata watoto wadogo wanaumwa magonjwa ya moyo ila kwa upande wao mara nyingi huwa ni magonjwa ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo kutokukaa katika mpangilio wake lakini pia kuna ambao wanayapata ukubwani na huwa ni matatizo ya valvu”.

“Tangu maadhimisho ya siku ya moyo yalipoanza  mara nyingi watu huwatazama watu wazima na kusahau watoto wadogo, ndio maana tumeona kama taasisi tutoe zawadi kwa watoto na kuwarudishia tabasamu. Ninaiomba jamii siku kama ya leo kukumbuka watu wote iwe ni kwa mtoto ambaye hajazaliwa au aliyezaliwa mwenye ugonjwa wa moyo na yule mkubwa wote ni sawa inatupasa kuwakumbuka”, alisema Dkt. Kubhoja.

Naye Mainda Hamu ambaye ni Afisa Muuguzi  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alisema wao kama wauguzi wamekuwa wakikaa muda mwingi na watoto wodini wamepata faraja kuona watoto wamepata zawadi ambazo zimewafanya watabasamu pia wazazi wao wamefurahi kupata mahitaji ya muhimu ya kila siku ambayo yatawasaidia wakiwa hospitali.

“Watoto na wazazi wao wamefurahi siku hii ya leo imekuwa faraja kwao kwani kuwapatia watoto zawadi za kuchezea na mahitaji yao ya muhimu ya kila siku wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani ni jambo jema linaloleta upendo na faraja kwa wagonjwa”, alisema Mainda.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenzake Zuhura Mkamba mama mzazi wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo aliwashukuru wafanyakazi wa  JKCI kwa kuwapa zawadi na kusema kuwa wamepata faraja kuona madaktari na wahudumu wengine wa afya wanajitoa na kuwapa zawadi wao na  watoto wao.

“Licha ya wafanyakazi wa hospitali hii kutuhudumia katika matibabu lakini pia wametupatia zawadi  jambo hili ni la kibinadamu sana ninawaomba watu wengine waige mfano na kuwakumbuka wagonjwa waliopo mahospitalini ili kuwapa faraja”.

Please follow and like us:
Pin Share