Dkt.Mpango afungua maonesho ya Nane Nane Mbeya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Geofrey Mkamilo juu kutumia tafiti kuinua mazao mbalimbali nchini ikiwemo zao la parachichi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma wakati akitembelea Banda la Wizara ya Kilimo katika Maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitembelea Mabanda mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza Mkurugenzi wa Ranchi ya Mbogo Pirmohamed Mulla wakati alipotembelea banda la Ranchi hiyo katika maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya leo tarehe 1 Agosti 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya kufungua maonesho ya Nanenane 2022 leo tarehe 1 Agosti 2022.