Na Lydia Lugakila, JamhuriMedia, Kagera

Mkulima na mchumi kutoka Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera Evance Emanuel Kamenge amesema kuwa Rais Samia ni kiongozi wa mfano na wa kupongezwa kwani ameleta mabadiliko makubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani CCM ya sasa sio kama ya zamani.

Kamenge ametoa kauli hiyo wakati Akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa namna gani anavyokitazama chama hicho kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Kamenge amesema Chama cha mapinduzi (CCM) kinampa faraja kubwa yeye kama kijana baada ya kuona Rais Samia anavyokiongoza kwa mabadiliko makubwa ikiwemo kurejesha nidhamu na msimamo mzuri.

“Chama hiki kimewapa vijana nafasi ngazi za juu za chama na Serikali, chama kimetoa somo kwa vyama vyama vingine”amesema Kamenge.

Kamenge ameongeza kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimekuwa kikisukuma agenda zake kwa vitendo na ni chama ambacho kimekataa na kimepinga rushwa ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kinapobaini wanachama wake na Viongozi wameshiriki katika vitendo vya Rushwa kwa ushahidi mzuri.

Aidha amesema kuwa jambo lililompa faraja yeye kama kijana ni pale alipoona chama kimeweza kufanya makosa pahala na kujirekebisha chenyewe na kikapokea maoni ya wanachama.

Hata hivyo Kamenge amesema kuwa kutokana na uongozi mzuri wa Rais Samia anaona siku za mbele chama hicho kitaongoza Taifa la Tanzania kwa mafanikio makubwa.