Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Mbeya

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa inaangalia usalama wa mafuta kwa watumiaji hivyo kufanya biashara ya mafuta bila leseni ni kosa la kisheria.

Imesema kuwa kanuni za uendeshaji wa biashara ya mafuta ya rejareja za mwaka 2022 zinamtaka mafanyabiashara ya mafuta ya petroli wa rejareja aombe leseni kutoka katika mamlaka hiyo.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la EWURA katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Akizungumza katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya,Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa AWURA Titus Kaguo amesema kuwa upo utaratibu wa kuomba leseni ya rejareja ya biashara ya mafuta lengo ikiwa kulinda usalama wa mafuta kwa watumiaji.

“Kuna utaratibu wa uombaji leseni wa rejareja ya biashara ya mafuta lengo likuwa ni kulinda usalama wa mafuta kwa watumiaji,pia kuna taarifa muhimu ambazo zitasaidia muhusika kukamilisha maombi yake,” amesema.

Kaguo amesema taarifa muhimu zinazohitajika kuomba leseni ni nakala ya nyaraka za usajili wa kampuni au leseni ya biashara, Hati ya Miliki ya Kiwanja palipojengwa kituo cha mafuta au udhibitisho mamlaka husika iliyoruhusu ujenzi wa kituo hicho , Kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri au Manispaa husika , Cheti cha tathimini ha athari ya mazingira , Nakala ya Cheti cha Mlipa kodi, Nakala ya cheti cha zimamoto.

Amesema utaratibu mwingine kibali cha ujenzi kutoka EWURA kwa vituo vilivyojengwa baada ya Aprili 2009, Orodha ya miundombinu iliyopo katika eneo , Mchoro wa Kituo ambao umesainiwa na mhandisi aliyesajiliwa na Baraza la Wahandisi Tanzania, Stakabadhi ya malipo ya ada na maombi ya kibali cha ujenzi ambayo ni 500, 000

By Jamhuri